728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, August 17, 2016

    MAN CITY YAFANYA MAUAJI MCHUJO LIGI YA MABINGWA ULAYA,AGUERO APIGA 3 AKOSA PENATI 2


    Bucurest,Romania.

    LICHA ya kukosa mikwaju miwili ya penati,Sergio Aguero,amefunga mabao matatu (Hat Trick) na kuiwezesha Manchester City kuibuka na ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Steaua Bucharest ya Romania katika mchezo wa kwanza wa mchujo wa kuwania kufuzu katika hatua ya makundi ya michuano ya klabu bingwa Ulaya maarufu kama UEFA Champions League.

    Katika mchezo huo uliofanyika usiku huu katika uwanja wa Arena Naţionala huko Bucurest,Romania,David Silva,alianza kuifungia Manchester City bao la kuongoza dakika ya 13 kisha Aguaero akaongeza matatu dakika za 41,78 na 89.Bao jingine limefungwa na Nolito dakika ya 49.



    Aguero akosa penati mbili.

    Aidha katika mchezo huo ilishuhudiwa,Sergio Aguero,akikosa mikwaju miwili ya penati ambayo ingeipatia Manchester City ushindi mnono zaidi.Penati ya kwanza ilipatikana baada ya Raheema Sterling kufanyiwa madhambi na Muniru Sulley huku ya pili ikipatikana baada ya Aleksandar Kolarov kuangushwa na Gabriel Enache 

    Timu hizo zitarudiana tena siku ya Jumatano Agosti 24 katika uwanja wa Etihad,Manchester na timu itakayokuwa imepata ushindi katika matokeo ya jumla itakuwa imefuzu hatua ya makundi.

    Vikosi

    Steaua XI: Niță, Tamaş, Hamroun,Stanciu, Muniru Sulley, Toşca, Golubović,Momčilović, Enache, Popa

    City XI: Caballero, Zabaleta, Otamendi,Stones, Kolarov, Fernandinho, De Bruyne,Silva, Nolito, Sterling,Aguero.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MAN CITY YAFANYA MAUAJI MCHUJO LIGI YA MABINGWA ULAYA,AGUERO APIGA 3 AKOSA PENATI 2 Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top