728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, August 16, 2016

    HIKI NDICHO KITUO CHA LUNINGA KITAKACHOONYESHA LIVE MCHEZO WA NGAO YA JAMII KATI YA YANGA NA AZAM,SIYO AZAM TV


    Dar Es Salaam,Tanzania.

    KITUO cha Luninga cha Agape Television Network (ATN) kimepata haki ya kuonesha moja kwa moja mchezo wa Ngao ya Hisani kati ya timu ya Yanga na Azam FC utakaofanyika kesho Jumatano kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kuanzia saa 10 jioni.

    Mkurugenzi wa michezo wa ATN Denis Msemwa amesema wamejipanga kurusha mchezo huo ambao utakuwa na muonekano bora yaani HD huku matukio yote muhimu yakionekana.

    Aidha Msemwa alisema pia vyombo vyengine vya habari vitaruhusiwa kurekodi dakika 15 za mwanzo na 15 za mwisho ili kuweza kutumia katika taarifa za habari ila baada ya mchezo wanaweza kupata CD ya mechi nzima.

    Kwa upande wake Ofisa Habari wa TFF Alfred Lucas amesema endapo mchezaji ataonywa kwa kadi katika mchezo huo adhabu hiyo itaendelea hadi kwenye mechi za ligi kuu kwa mujibu wa kanuni za ligi kuu ya Vodacom.

    "Kama mnakumbuka mchezaji Erasto Nyoni alioneshwa kadi ya njano katika mchezo kama huu mwaka jana ikaigharimu Azam hadi kupokwa alama kwahiyo wachezaji wanatakiwa wawe makini,"alisema Lucas.

    Viingilio katika mchezo huo vitakuwa kama ifuatavyo;VIP A 20,000,VIP B na C itakuwa 15,000 huku mzunguko ikiwa ni 5,000.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: HIKI NDICHO KITUO CHA LUNINGA KITAKACHOONYESHA LIVE MCHEZO WA NGAO YA JAMII KATI YA YANGA NA AZAM,SIYO AZAM TV Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top