728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, August 08, 2016

    OLIMPIKI:WENYEJI BRAZIL BADO NGOMA NGUMU WAPATA SARE NYINGINE,MASHABIKI WAZOMEA TENA

    Brasilia, Brazil.

    Kwa mara ya pili mfululizo wenyeji Brazil wamejikuta wakitoka uwanjani kichwa chini.Wamevimba kwa hasira hii ni baada ya timu yao ya taifa ya soka kushindwa kupata ushindi katika michuano ya soka ya Olimpiki inayoendelea nchini humo.

    Muda mchache uliopita Brazil imelazimishwa sare ya bila kufungana na Iraq katika mchezo wa kundi A uliochezwa katika uwanja wa taifa wa nchi hiyo huko Brasilia.

    Matokeo ambayo ambayo ni ya kwanza tangu mwaka 1972 kwa Brazil kucheza michezo miwili mfululizo ya Olimpiki bila kufunga bao yameibua hasira kali kutoka kwa mashabiki wa timu hiyo ambao waliamua kuizomea timu hiyo huku akiimba jina la Iraq na kuwasifu wachezaji wa timu hiyo ya Asia.

    Wapo baadhi ya mashabiki wa Brazil ambao walisikika wakiliimba jina la staa wa kike wa nchi hiyo Marta ambaye ameipeleka robo fainali timu yao ya wanawake na kutania aletwe kuwaonyesha wanaume jinsi ya kufunga mabao.

    Kwa matokeo hayo Brazil imefikisha pointi mbili na ili iweze kufuzu robo fainali italazimika kuwafunga vinara wa kundi hilo la A,Denmark,wenye pointi nne.Iraq ina pointi mbili pia na mkiani iko Afrika kusini yenye pointi moja pekee.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: OLIMPIKI:WENYEJI BRAZIL BADO NGOMA NGUMU WAPATA SARE NYINGINE,MASHABIKI WAZOMEA TENA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top