728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, August 08, 2016

    NIGERIA YAIBUTUA SWEDEN NA KUTINGA ROBO FAINALI OLIMPIKI

    Manaus,Brazil.

    NIGERIA imekuwa timu ya kwanza kutoka kundi B kutinga hatua ya robo fainali ya michuano ya soka ya Olimpiki kwa upande wa wanaume baada ya kuitungua Sweden kwa bao 1-0 katika mchezo mkali uliochezwa katika uwanja wa Amazonia Arena huko Manaus,Brazil.

    Bao pekee la mchezo huo limefungwa dakika ya 40 kwa kichwa na Mshambuliaji Mrefu,Sadiq Umar.Umar alifunga bao hilo akiunganisha krosi safi toka kwa Stanley Amuzie na kufanya mchezo uishe kwa Nigeria kutoka kifua mbele kwa bao hilo moja.

    Matokeo hayo yameifanya Nigeria ifikishe pointi sita na kutinga robo fainali.Katika mchezo wa kwanza Nigeria ilichapa Japan kwa mabao 5-4.

    Nigeria itarejea tena dimbani siku ya Jumanne kuhitimisha michezo yake ya kundi B kwa kucheza na Colombia huku Sweden wao wakipepetea na Japan siku hiyo hiyo.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: NIGERIA YAIBUTUA SWEDEN NA KUTINGA ROBO FAINALI OLIMPIKI Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top