Gothenburg,Sweden.
Arsenal imetoka nyuma na kuifunga Manchester City mabao 3-2 katika mchezo mkali wa kirafiki uliomalizika hivi punde huko Gothenburg,Sweden.
Mabao yaliyoipa ushindi Arsenal katika mchezo huo yamefungwa na Alex Iwobi, Theo Walcott na Chuba Akpom.
Manchester City imepata mabao yake kupitia kwa Sergio Aguero na Kelechi Iheanacho aliyefunga kwa kichwa akiunganisha krosi ya Jesus Navas.
Aidha katika mchezo huo Arsenal imepata pigo baada ya beki wake Gabriel Paulista kuumia vibaya kufuatia kugongana na mshambuliaji wa Manchester City,Kelechi Iheanacho na kulazimika kutolewa uwanjani akiwa kwenye machela.
0 comments:
Post a Comment