London,Uingereza.
ANDRE 'DEDE' AYEW ameipa pigo kubwa klabu yake mpya ya Westham United hii ni baada ya leo kuripotiwa kuwa atakuwa nje ya dimba kwa kipindi cha miezi minne kutokana na kuumia paja.
Ayew,26,alipata jeraha hilo Jumatatu Usiku katika mchezo ambao klabu yake ya Westham United ilichapwa na Chelsea kwa mabao 2-1 katika mchezo wa kwanza wa ligi kuu England uliochezwa katika uwanja wa Stamford Blidge.
Katika mchezo huo Ayew alidumu kwa dakika 30 tu za kipindi cha kwanza na kulazimika kutolewa na nafasi yake kuchukuliwa na Gokhan Tore baada ya kushindwa kuendelea na mchezo.
Kwa mujibu wa Mkuu wa Idara ya masuala ya kitabibu wa Westham United,Stijn Vandenbroucke,Ayew analazimika kuwa nje kwa kipindi hicho kutokana na jeraha lake kuhitaji kufanyiwa upasuaji ili kupatiwa ufumbuzi.
Ayew alijiunga na Westham United mapema mwezi huu kwa ada ya rekodi ya klabu hiyo ya £20.5m akitokea Swansea City na kuumia kwake ni pigo kubwa kwa klabu hiyo ambayo msimu huu imepania kufika mbali ikiwezekana kutwaa ubingwa wa ligi kuu England.
0 comments:
Post a Comment