728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, July 03, 2016

    MARIO BALOTELLI BADO HAJAKATA TAMAA KUTWAA BALLON D'OR

    Liverpool,England.

    STAA wa Liverpool,Mario Balotelli,amesisitiza kuwa bado ana matumaini kuwa siku moja atatwaa tuzo ya mchezaji bora wa dunia maarufu kama Ballon d'Or licha ya kwamba katika kipindi cha misimu miwili iliyopita hakuwa katika kiwango bora cha uchezaji.

    Balotelli,25,ameyasema hayo jana Jumamosi baada ya kurejea Liverpool kuanza mazoezi ya kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu akitokea AC Milan alikokuwa akicheza kwa mkopo.

    Akiongea na Corriere della Sera,Balotelli,amekiri kwamba ameshindwa kuonyesha makali yake katika kipindi cha miaka miwili iliyopita lakini amesisitiza kuwa hali hiyo bado haimfanyi akate tamaa ya kutwaa Ballon d'Or.

    Amesema "Sijafanya vizuri katika miaka ya hivi karibuni.Bado naweza kufanya vizuri zaidi,lakini inahitaji muda.

    Katika mzani/scale ya moja mpaka 10,nimefika tano.Nitajitahidi niweze kufika kumi kwani hilo ndilo lengo langu.

    "Nataka kutwaa Ballon d'Or.Nimekuwa na ndoto hii kwa kipindi kirefu.Najua watu watanicheka wakisikia kuwa nataka kutwaa Ballon d'Or licha ya kutokuwa katika kiwango bora.Lakini jambo la msingi hapa ni kuwa tayari nimeshayajua makosa yangu,bado sijachelewa.

    Kauli hiyo ya Balotelli inaweza kuonekana kuwa ni kichekesho kitupu kwa sasa kwani staa huyo wa zamani wa Manchester City amejikuta akikosa nafasi katika vilabu vya Liverpool na AC Milan ambavyo vimekuwa vikipokezana kumtumia katika siku za hivi karibuni.Tusubiri tuone.



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MARIO BALOTELLI BADO HAJAKATA TAMAA KUTWAA BALLON D'OR Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top