728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, July 03, 2016

    LECEISTER CITY YAMNASA KANTE MWINGINE KWA DAU LA REKODI

    Leceister,England.

    Mabingwa wa Ligi Kuu England,Leicester City wameendelea kukiimarisha kikosi chao tayari kwa msimu ujao wa michuano mbalimbali baada ya leo hii kukamilisha usajili wa kiungo mkabaji,Nampalys Mendy,kutoka Nice ya Ufaransa kwa ada rekodi ya £13m.

    Mendy,24,amesaini mkataba wa miaka minne wa kuwatumikia wakali hao wa King Power baada ya kufuzu vipimo vyake vya afya katika kliniki ya klabu hiyo.

    Mendy ambaye kiuchezaji anafananishwa na kiungo mwingine wa klabu hiyo,NG'olo Kante,amekuwa mchezaji ghari zaidi kuwahi kusajiliwa na klabu hiyo akivunja rekodi iliyowekwa na Leonardo Ulloa, mwaka 2014 aliposajiliwa akitikea Brighton and Hove Albion kwa ada ya £10m.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: LECEISTER CITY YAMNASA KANTE MWINGINE KWA DAU LA REKODI Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top