728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, July 03, 2016

    ARSENAL YAMNASA TAKUMA WA JAPAN

    London, England.

    Arsenal imeonyesha bado haijapoteza makali yake katika kuvumbua vipaji hii ni baada ya mchana huu kutangaza kufikia makubaliano ya kumsajili mshambuliaji wa Japan, Takuma Asano,21,kutoka Sanfrecce Hiroshima.

    Akithibitisha habari hiyo kupitia mtandao Rasmi wa klabu hiyo,Meneja Arsene Wenger amekiri Arsenal kushinda mbio za kumuwania mshambuliaji huyo na kusisitiza kuwa Takuma ni mshambuliaji kinda mwenye kipaji kikubwa na atakuwa msaada mkubwa hapo baadae.

    Takuma mwenye uwezo wa kucheza nafasi zote za mbele ameichezea Sanfrecce Hiroshima jumla ya michezo 56 akifanikiwa kufunga mabao 11pia akiwa sehemu ya kikosi hicho kilichotwaa ubingwa wa Ligi kuu ya Japan (J-League) mara mbili mwaka 2013 na 2015.

    Wakati huohuo habari zinasema Takuma atafanyiwa vipimo vya afya yake kesho Jumatatu na baada ya hapo atatolewa kwa mkopo katika vilabu vingine vya Ulaya ili kuongeza uzoefu.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: ARSENAL YAMNASA TAKUMA WA JAPAN Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top