728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, July 03, 2016

    CHELSEA YASAJILI MTAMBO WA MABAO TOKA UFARANSA

    London, England.

    Chelsea imetangaza kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa Ubelgiji ,Michy Batshuayi,kutoka Marseille ya Ufaransa kwa ada ya £33.2m.

    Batshuayi,22,amesaini mkataba wa miaka mitano wa kuitumikia miamba hiyo ya Stamford Bligde na atakuwa akilipwa mshahara wa £70,000 kwa wiki.

    Akifanya mahojiano baada ya kusaini mkataba, Batshuayi,amesema “Nimefurahi kujiunga na moja kati ya vilabu vikubwa Ulaya.Nimefungua ukurasa mpya katika maisha yangu.Natumaini kuwa nitaisaidia Chelsea kutwaa mataji mengi katika kipindi chote nitakachokuwa Stamford Bridge.

    “Eden Hazard na Thibaut Courtois wameniambia mambo mengi mazuri kuhusu klabu hii,Ukizingatia Antonio Conte nae anakuja nadhani nimekuja katika kipindi kizuri.Hii ni fursa nzuri kwangu na kwa familia yangu,nasubiri kwa hamu kuanza kucheza Premier League"

    Batshuayi alianzia soka lake katika klabu ya Standard Liège kabla ya mwaka 2014 kujiunga na Marseille ambapo katika msimu wake wa kwanza aliifungia klabu hiyo ya Stade Velodrome mabao 15. 

    Msimu uliofuta yaani 2015/2016 aliifungia Marseille mabao 26 katika michuano yote huku 17 yakiwa ni katika Ligi daraja la kwanza Ufaransa maarufu kama Ligue 1.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: CHELSEA YASAJILI MTAMBO WA MABAO TOKA UFARANSA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top