728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, July 05, 2016

    KIUNGO MPYA LIVERPOOL APATA KIBARI SASA RUKSA KUKIPIGA ENGLAND

    Liverpool,England.

    LIVERPOOL imeshinda vita ya nje ya uwanja hii ni baada ya kiungo wake mpya toka Serbia,Marko Grujic kufanikiwa kupata kibari cha kufanyia kazi nchini England.

    Grujic,20,amepata kibari hicho Jana Jumatatu baada ya mamlaka zinazohusika kuridhika na maombi pamoja na maelezo yaliyotolewa na Liverpool kupitia kwa kocha wake Jurgen Klopp katika shauri lililosikilizwa jijini Manchester.

    Grujic ambaye atakuwa akivalia jezi namba 16 alijiunga na Liverpool mwezi Januari mwaka huu kwa ada ya £5.1m akitokea klabu ya Red Star Belgrade ya nyumbani kwao Serbia lakini kutokana na kushindwa kupata kibari cha kufanyia kazi nchini England alilazimika kubaki klabuni hapo kwa mkopo.

    Msimu uliopita,Grujic,aliichezea Red Star Belgrade jumla ya michezo 30 akifunga mabao sita na kupika mengine saba na alikuwa nguzo katika kikosi cha vijana cha Serbia kilichotwaa kombe la dunia la vijana la U20 kwa kuichapa Brazil katika fainali zilizochezwa huko nchini New Zealand.



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: KIUNGO MPYA LIVERPOOL APATA KIBARI SASA RUKSA KUKIPIGA ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top