Dar es Salaam,Tanzania.
klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC , leo imemshusha mshambuliaji kutoka Ivory Coast , Ibrahima Fofana tayari kabisa kufanya majaribio .
Azam FC kwasasa wapo kwenye mchakato wa kukifanyia marekebisho kikosi chake na moja ya eneo walilolimulika ni kuboresha eneo la ushambuliaji kwa kusajili
washambuliaji wapya wawili wenye viwango vya juu.
Fofana (26), ametua nchini akitokea timu ya Union Sportive de Ben Guerdane ya Tunisia aliyokuwa akiichezea msimu uliopita uliomalizika Juni 14 mwaka huu.
Nyota huyo mwenye uwezo wa kucheza namba 9, 7 na 11, kabla ya kujiunga na
timu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu ya Tunisia (Ligue 1) alikuwa akikipiga kwa miamba ya Ivory Coast Asec Mimosas tokea mwaka 2013 hadi 2015.
Fofana ataanza rasmi majaribio yake keshokutwa Ijumaa wakati kikosi cha Azam FC kitakapoendelea na mazoezi yake,ambapo kesho Alhamisi ni siku ya
mapumziko.
Mshambuliaji huyo anaungana na makipa wawili wa kigeni, Daniel Yeboah (Ivory Coast) na Juan Jesus Gonzalez (Hispania),wanaoendelea kufanya majaribio ndani ya
Azam FC wakigombea nafasi moja ya usajili ya golikipa.
0 comments:
Post a Comment