Turin,Italia.
KLABU ya Juventus imemsajili Mlinzi wa Morocco,Medhi Benatia,kutoka Bayern Munich kwa Mkopo wa Mwaka Mmoja kwa Ada ya €3m (£2.5m).
Benatia,29,ameamua kujiunga na Juventus baada ya Bayern Munich kumwambia kuwa hayumo katika mipango ya klabu hiyo hasa baada ya ujio wa mlinzi wa Ujerumani,Mats Hummels,kutoka Borussia Dortmund.
Katika uhamisho huo wa Mkopo,Juventus,pia imepewa mwanya wa kumsajili moja kwa moja Benatia kwa ada ya €17m (£14.3m) hapo mwishoni mwa msimu ujao.
0 comments:
Post a Comment