Vienna,Austria.
CHELSEA imeyaanza vibaya Maandalizi ya Msimu Mpya wa Ligi Kuu England baada ya jioni ya Leo kuchapwa mabao 2-0 na Rapid Vienna ya Austria Katika mchezo wa Kimataifa wa Kirafiki uliochezwa katika uwanja wa Allianz Stadion huko Vienna, Austria.
Mabao yaliyotia doa maandalizi ya Chelsea yamefungwa dakika za 8 na 82 kupitia kwa Joelinton pamoja na Tomi Correa.
Chelsea itarejea tena uwanjani siku ya Jumatano Julai 20 katika mji wa Velden kucheza mchezo mwingine wa kirafiki lakini safari hii itakuwa dhidi ya WAC RZ Pellets.
VIKOSI
Chelsea: Begovic, Ivanovic, Djilobodji, Terry,Baba Rahman (Aina 46), Obi (Chalobah 58),Matic (Traore 77), Loftus-Cheek (Oscar 46),Moses (Atsu 80), Willian (Kenedy 72), Diego
Costa (Remy 72)
Rapid Vienna : Novota (Strebinger h/t),Schosswendter (Dibon), Schrammel (Auer 84), S.Hofmann (c) (Murg 55), Grahovac,Szanto (Nutz 81), M.Hofmann (Sonnleitner 81),Schobesberger (Entrup 84), Schaub (Schwab 77), Pavelic, Joelinton (Tomi).
0 comments:
Post a Comment