Alexandria,Misri.
MATUMAINI ya Klabu ya Al Ahly ya Misri kutinga hatua ya Nusu Fainali ya Michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika yameyeyuka baada ya Jumamosi Usiku ikiwa nyumbani Alexandria kulazimishwa sare ya bila kufungana na Wydad Casablanca ya Morocco katika Mchezo Mkali wa Robo Fainali wa Kundi A uliochezwa katika Uwanja wa Borg El-Arab jijini Alexandria.
Sare hiyo inaiacha Al Ahly ikiendekea kuweka makazi yake ya kudumu mkiani mwa kundi A hii ni baada ya kujikusanyia pointi moja pekee mpaka sasa licha ya kucheza michezo mitatu ya hatua ya makundi.
Wydad Casablanca inaongoza kundi A ikiwa na pointi saba, Zesco United ni ya pili ikiwa na pointi sita,ASEC Mimosas ni ya tatu ikiwa imejikusanyia pointi tatu mpaka sasa.
Michezo ya marudiano ya Kundi A inatarajiwa kuchezwa Julai 27 ambapo Wydad Casablanca watakuwa wenyeji wa Al Ahly huko Casablanca,Morocco huku Zesco United wakisafiri mpaka Abidjan,Ivory Coast kwenda kuvaana na ASEC Mimosas.
0 comments:
Post a Comment