Cairo,Misri.
Shirikisho la Soka Barani Afrika, CAF kupitia kwa bodi yake ya masuala ya nidhamu imeipiga klabu ya Yanga faini ya dola za kimarekani 10, 000 sawa na zaidi ya milioni za shilingi za Tanzania.
Faini hio ya CAF imetolewa kutokana wachezaji wa Yanga kupinga maamuzi ya mwamuzi katika mchezo wa marudiano wa mchujo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Esperanca Sagrada ya Angola.
Hata hivyo, Yanga imepewa nafuu ya kulipa nusu ya kiasi hicho na kutakiwa kulipa kiasi kingine endapo tu itarudia kosa hilo.
katika mchezo, Sagrada walipewa penati dakika ya mwisho ya pambano pamoja na nahodha wa Yanga kutolewa nje kwa kadi nyekundu.
Hata hivyo Yanga ilifanikiwa kufuzu kwa
hatua ya makundi baada ya kufungwa bao 1-0 na hivyo kusonga mbele kwa ushindi wa jumla wa mabao 2-1.
0 comments:
Post a Comment