Brussels, Ubelgiji.
CHAMA cha Soka cha Ubelgiji,KBVB,kimemfuta Kazi aliyekuwa Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya nchi hiyo,Marc Wilmots,kufuatia kuondolewa mapema katika michuano ya Euro 2016 iliyofikia tamati yake wiki iliyopita.
KBVB imeamua kuachana na Wilmots baada ya kushuhudia timu yake iliyokuwa imesheheni mastaa kibao ikiishia hatua ya robo fainali baada ya kukubali kichapo cha mabao 3-1 toka kwa Wales katika mchezo wa robo fainali.
Ikiwa chini ya Wilmots,Ubelgiji ilifanikiwa kushinda michezo 34 kati ya 51.Pia ilifanikiwa kutoka sare mara nane.Wilmots ameiacha Ubelgiji ikishika nafasi ya pili katika ubora wa viwango vya soka Ulimwenguni kutoka katika nafasi ya 54 ilikuwa ikiishikilia mwaka 2012 wakati anakabidhiwa timu hiyo.
0 comments:
Post a Comment