728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, February 08, 2016

    ZOUMA NJE MIEZI SITA

    London,England.

    Klabu ya Chelsea imepata pigo baada ya mlinzi wake wa kutumainiwa Mfaransa Kurt Zouma kuripotiwa kuwa atakuwa nje ya uwanja kwa kipindi cha miezi sita baada ya kupata jeraha la goti katika mchezo wa jumapili wa ligi kuu England dhidi ya Manchester United uliofanyika katika uwanja wa Stamford Blidge.

    Zouma,21 aliumia goti lake la mguu wa kulia kufuatia kutua vibaya baada ya kucheza mpira wa juu wa kichwa na kisha kushindwa kuendelea na mchezo baada ya kuzidiwa na maumivu.

    Kufuatia jeraha hilo Zouma atakosa michezo yote iliyosalia ya ligi kuu pamoja na michuano ya Ulaya/Euro inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi lake huko Ufaransa mwezi Juni.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: ZOUMA NJE MIEZI SITA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top