728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, February 08, 2016

    KAMUSOKO MCHEZAJI BORA LIGI KUU BARA KWA MWEZI DISEMBA


    Mchezaji Thaban Kamusoko amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom kwa mwezi Disemba, 2015 baada ya kumshinda mchezaji mwenzake wa Yanga (Amissi Tambwe).

    Kamusoko ameisaidia timu yake ya Yanga katika michezo iliyochezwa mwezi Disemba kwa kushiriki dakika zote katika michezo mitatu iliyochezwa mwezi wa Disemba.

    Kwa kuchaguliwa kwake kuwa mchezaji bora wa wa mwezi Disemba, Kamusoko atakabidhiwa zawadi ya fedha taslimu shilingi milioni moja (1,000,000) kutoka kwa wadhamini wa ligi Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: KAMUSOKO MCHEZAJI BORA LIGI KUU BARA KWA MWEZI DISEMBA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top