728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, February 02, 2016

    MALINZI AIPONGEZA RUVU SHOOTING KWA KUREJEA LIGI KUU

    Dar es salaam,Tanzania.

    Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kupitia kwa Rais wake, Jamal Malinzi
    ametuma salamu za pongezi kwa klabu ya Ruvu Shooting kwa kufanikiwa kupanda Ligi
    Kuu ya Vodacom msimu ujao.
    Malinzi ametuma salamu hizo kwa Mwenyekiti wa klabu ya Ruvu Shooting, Col. Charles
    Mbuge, viongozi, benchi la ufundi na wachezaji na kuwataka kujipanga kwa
    maandalizi ya nguvu msimu ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom.

    Ruvu Shooting imekua timu ya kwanza kupanda ligi kuu msimu huu baada ya jana
    kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Lipuli FC mjini Iringa na kufikisha alama 31
    ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote kutoka katika hilo la B.

    Washindi wawili kutoka maundi ya A, na B wataungana na Ruvu Shooting kupanda Ligi
    Kuu ya Vodacom msimu ujao huku timu zote zikiwa zimebakiza michezo miwili miwili kabla ya kumalizika kwa ligi daraja la kwanza
    msimu huu.



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MALINZI AIPONGEZA RUVU SHOOTING KWA KUREJEA LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top