London,England.
Mlinda mlango Peter Cech ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi wa Arsenal kwa mwezi Januari baada ya kuwabwaga kwa kura nyingi washambuliaji Olivier Giroud na Joel Campbell.
Cech,33 aliyetua Arsenal mwezi Julai mwaka jana akitokea Chelsea ametwaa tuzo hiyo baada ya kupata kura 47.4 huku nafasi ya pili ikichukuliwa na Giroud aliyepata kura 18.9 na nafasi ya tatu ikienda kwa Campbell aliyepata kura 8.9.
Washindi wa miezi iliyopita
August: Francis Coquelin
September: Theo Walcott
October: Mesut Ozil
November: Mesut Ozil
December: Mesut Ozil
January: Petr Cech
0 comments:
Post a Comment