Manchester,England.
Manchester United imeripotiwa kuwa mbioni kufanya usajili mwingine wa kushitukiza kwa kumsajili kiungo/mshambuliaji wa Bayer Leverkusen Hakan Calhanoglu.
Hakan Calhanoglu,21 raia wa Uturuki mtaalamu wa mipira ya adhabu (free-kicks) inadaiwa ametengewa kitita cha £27m ili atue Old Trafford leo kabla ya dirisha la usajili halijafungwa baadae leo usiku.
Manchester United ina matumaini ya kufanikisha dili hilo baada ya jana kuiuzia Leverkusen mshambuliaji wake Mmexico Javier Hernandez "Chicahrito"
0 comments:
Post a Comment