728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, September 14, 2015

    SASA NI RASMI:SPURS YAMTEMA EMANUEL ADEBAYOR

    London,England.

    Mshambuliaji Emanuel Adebayor ameachana rasmi na Tottenham Hotspurs na sasa ni mchezaji huru.Taarifa kutoka kwa Adebayor na Tottenham zinasema uamuzi huo umefikiwa baada ya pande zote mbili kufikia maridhiano ya kufanya hivyo.

    Kwa kipindi kirefu sasa kumekuwa na msuguano wa chini chini kati ya Emanuel Edebayor na Tottenham hasa kocha mkuu Maurcio Pochettino mpaka kufikia hatua kwa mshambuliaji huyo wa zamani wa Monaco,Arsenal na Manchester City kuachwa katika vikosi viwili vinavyoiwakilisha Tottenham katika michuano ya ligi kuu pamoja na michuano ya Ulaya (Europa Ligi) huku kubwa zaidi ikiwa ni kunyimwa namba ya jezi.

    Msuguano kati ya Tottenham na Adebayor ulipamba moto katika majira yaliyopita ya usajili baada ya Adebayor kukataa kujiunga na Aston Villa kwa mkopo akitaka kwanza alipwe £5m ili aachane jumla na Tottenham vinginevyo asingehama.

    Adebayor alijiunga na Tottenham mwaka 2011 kwa ada ya £5m akitokea Manchester City na kufanikiwa kufunga magoli 42.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: SASA NI RASMI:SPURS YAMTEMA EMANUEL ADEBAYOR Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top