Sergio Busquets anafahamika kwa mambo mengi sana.Anafahamika kwa umahiri wa kuzuia,kupiga takling na pasi murua kabisa awapo uwanjani lakini linapokuja suala na mahusiano kidogo jamaa yuko tofauti na watu wengi.
Wakati watu wengi wakiamini kuwa ngono,ulevi ndiyo starehe kubwa zaidi Busquets yeye wala hana habari kabisa na jambo hilo.Akifanya mazungumzo na kituo cha Televisheni cha kwao Hispania katika kipindi cha El Hormiguero nyota huyo wa kiungo cha ulinzi cha FC Barcelona akijibu swali aliloulizwa kubwa kipi ni zaidi ya mpira na ngono bila kupepesa macho wala kuumauma maneno Busquets alijibu
"Kwenye mpira,furaha hudumu siku tatu mpaka nne lakini kwenye ngono hudumu dakika moja tu."
0 comments:
Post a Comment