Klabu ya Wolfsburg imeendeleza rekodi yake nzuri mbele ya Bayern Munich baada ya kuifunga kwa penati 5-4 miamba hiyo ya Bundesliga na kutwaa taji la Super Cup katika mchezo mkali uliopigwa usiku wa jana jumamosi katika dimba la Volkswagen Arena.
Katika mchezo huo ambao huashiria kuanza kwa ligi ya Ujerumani (Bundesliga) Bayern walianza kujipatia goli dakika ya 49 kupitia kwa winga wake Arjen Robben kabla ya wenyeji Wolfsburg kusawazisha dakika ya 89 kupitia kwa mshambuliaji Niklas Bendtner akiunganisha krosi safi ya kiungo Kevin De Bruyne.Mpaka dakika tisini zinaisha matokeo yalikuwa ni sare ya 1-1.
Bayern Munich waliokuwa wakilisaka taji hilo bila mafanikio tangu mwaka 2012 walilikosa tena baada ya penati ya kiungo wake Xabi Alonso kuzuiwa kwa miguu na mlinda mlango wa Wolfsburg Koen Casteels na matokeo kuwa 5-4 huku pongezi za dhati zikimuendea Bendtner kwani licha ya kusawazisha goli pia alifunga penati.
0 comments:
Post a Comment