Unamkumbuka Roy Keane yule nahodha wa zamani wa Manchester United?Yule aliyekuwa hapikiki chungu kimoja na nahodha wa zamani wa Arsenal Patrick Vieira?Sasa ameibuka na hili.
Akifanya mazungumzo na gazeti la Daily Star,Roy Keane amesema Arsenal ina wachezaji wazuri.Wenye tabia nzuri lakini tatizo lao ni kuwa wanapenda sana kujipiga picha "Selfie" kuliko kutwaa taji la ligi kuu (EPL)
Amesema "Wachezaji wa Arsenal wanapenda selfie,kujenga miili yako ionekane yenye mvuto "six packs" na kuweka mitindo mbalimbali ya nywele lakini linapokuja suala la kutwaa mataji kwao inakuwa ni hadithi tofauti.
"Kila mwaka sababu zimekuwa ni zile zile.Siku za karibuni Arsenal imejitahidi kununua wachezaji wazuri lakini sidhani kama kuna yeyote anayeweza kupata nafasi katika kikosi cha Chelsea"Alimaliza Roy Keane.
0 comments:
Post a Comment