Aranguiz:Baada ya kuondokewa na kiungo wake mahari Muargentina Esteban Cambiasso klabu ya Leicester City imeripotiwa kukubaliana dau la £10.5m na klabu ya Internacional ya Brazil kwa ajili ya kumsajili kiungo Mchile Charles Aranguiz.
Habari zaidi zinasema Leceister City imefungua majadiliano juu ya maslahi binafsi na nyota huyo aliyeipa Chile kombe la Copa America mwezi uliopita.Ikiwa mambo yataenda sawa Aranguiz atakuwa mchezaji ghari zaidi kusajiliwa na klabu hiyo akivuka dau la £9m lililotumiwa na klabu hiyo kumsajili mshambuliaji Kramalic hapo mwezi januari.
Wakati huohuo Leceister City pia imeshinda mbio za kuinasa saini ya kiungo mzoefu wa Napoli Gokhan Inler,31 baada ya ofa yake ya £3m kukubaliwa na klabu hiyo ya Seria A.
Baba Rahman:Klabu ya Augsburg ya Ujerumani imeonyesha nia ya dhati ya kutaka kumuuza mlinzi wake wa kushoto Mghana Baba Rahman kwenda klabu ya Chelsea baada ya kuripotiwa kukubali kumnunua mlinzi wa Karlsruhe Philipp Max.
Augsburg itamnunua mlinzi huyo kwa kitita cha €12m kutoka katika kitita cha €25m inachotarajia kukipata baada ya kumuuzaBaba Rahman kwa klabu ya Chelsea.
Baba Rahman aliyewahi kuvichezea vilabu vya Asante Kotoko na Dreams FC ameandaliwa mshahara wa £27,000 kwa wiki ikiwa atatua London kujiunga na Chelsea.
Birmingham,England.
Berbatov:Klabu ya Aston Villa imeripotiwa kuwa karibu kufanya usajili mwingine mkubwa wa kumsajili mshambuliaji mkongwe Dimitar Berbatov toka klabu ya Monaco ya Ufaransa.
Berbatov aliyewahi kukipiga na klabu ya Manchester United anatarajiwa kuwasili katika jiji la Birmingham kwenye makao makuu ya klabu ya Aston Villa jumatatu ijayo kwa ajili ya kufanyiwa vipimo vya afya.Habari za kuaminika zinadai ujio huo wa Berbaton umechangiwa kwa kiasi kikubwa na Stilian Petrov ambaye ni rafiki yake wa karibu na pia ni kocha msaidizi katika klabu hiyo.
0 comments:
Post a Comment