728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, August 05, 2015

    TETESI:CHICHARITO AOMBA KUPUNGUZIWA BEI AONDOKE UNITED,PEDRO KUCHEZA MCHEZO WA MWISHO LEO AKIWA NA JEZI YA BARCELONA,LACAZZETTE NIACHENI NIONDOKE MIEE

    Danish goalkeeper Anders Lindegaard has been told he can leave Manchester United on a free transfer 
    Lindegaard:Klabu ya Manchester United imemwambia mlinda mlango wake toka Denmark Anders Lindegaard,31 kuwa hana nafsi tena klabuni hapo hivyo yuko huru kuondoka bure kabisa.Lindegaard alijiunga na Manchester United mwaka 2010 akitokea klabu ya nyumbani kwao ya Aalesund na kufanikiwa kucheza jumla ya michezo 29 pekee.

    Donsah:Vilabu ya Chelsea na Juventus viko katika majadiliano na klabu ya Cagliari kwa ajili ya kusajili kiungo wake kinda Mghana Godfred Donsah,19.(Daily Express.)
                   
    Chicharito:Mshambuliaji wa klabu ya Manchester United Mmexico Javier Hernandez anajiandaa kutuma maombi rasmi ya kutaka klabu hiyo ipunguze bei ili aweze kutimka klabuni hapo.Henandez anaona bei ya £12m iliyowekwa kwa ajili yake ni kubwa mno.Vilabu vinavyomtaka nyota huyo ni  Tottenham na Westham.  (Daily Star)



     
    De Bruyne:Klabu ya Wolfsburg imetangaza kuwa iko tayari kumuuza nyota wake Kevin De Bruyne kwenda klabu ya Manchester City ikiwa tu matajiri hao wa ligi kuu nchini England watakuwa tayari kutoa kitita cha £50m.(Daily Mirror)



                        
    Lacazzette:Mshambuliaji Lyon Alexander Lcazzette huenda akaihama klabu hiyo baada ya kujikuta akiingia matatani baada ya kuonyesha kiwango kibovu katika mchezo wa jumamosi wa Super Cup dhidi ya PSG.Lacazette amelaumiwa kwa kuonyesha kiwango kibovu katika mchezo huo pamoja na ule dhidi ya Arsenal katika michuaano ya Emirates Cup.Taarifa toka Ufaransa zinadai tayari Lacazzette ameiambia klabu hiyo imuuze.(L'Equipe)


                      
    Baba Rahman:Wakala wa mlinzi wa klabu ya Augsburg Baba Rahman aitwaye Sascha Empacher amesema mteja wake tayari ameshafikia makubaliano binafsi na klabu ya Chelsea kilichobaki na vilabu hivyo viwili kufanya makubaliano juu ya bei yake.



    Pedro of FC Barcelona shoots past Milan Badelj

    Pedro:Gazeti la Marca la nchini Hispania limeripoti kuwa winga Pedro Rodriguez,27  ataichezea klabu ya Barcelona mchezo wa mwisho leo kabla ya kujiunga na klabu ya Manchester United.Barcelona leo usiku itajitupa uwanjani kuvaana na klabu ya AS Roma 
     
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: TETESI:CHICHARITO AOMBA KUPUNGUZIWA BEI AONDOKE UNITED,PEDRO KUCHEZA MCHEZO WA MWISHO LEO AKIWA NA JEZI YA BARCELONA,LACAZZETTE NIACHENI NIONDOKE MIEE Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top