728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, August 05, 2015

    MAYWEATHER AMTOSA KHAN, SASA KUZICHAPA NA BERTO


      Bondia asiyepigika, Floyd Mayweather amemtosa Mwingereza, Amir Khan na sasa atapigana na bingwa mwingine.
    Floyd Mayweather

    Hilo litakuwa ni pambano la 49 la Mayweather ambaye hajapigwa hata mara moja na linatarajia kufanyika Septemba 12 jijini Las Vegas, Marekani.
    Mmarekani huyo anatarajia kuzichapa na Andre Berto ambaye pia ni bingwa wa uzito huo.




    Pambano lake la mwisho lilikuwa ni dhidi ya Manny Paqcuiao na ushindi wake ulizua mjadala mkubwa mara tu baada ya pambano kwenye ukumbi wa MGM Grand Garden Arena.
    Mayweather anakaribia mapambano 50 bila ya kushindwa na yeye amekuwa akisema kwamba pambano lijalo ndilo la mwisho ingawa watu wake wa karibu wanasema atacheza hadi mapambano 50.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MAYWEATHER AMTOSA KHAN, SASA KUZICHAPA NA BERTO Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top