Leo ni leo katika dimba la Boris Paichadze Dinamo Arena,Georgia pale miamba ya La liga FC Barcelona na FC Sevilla itakapovaana kuwania Super Cup ya vilabu bingwa Ulaya.Mtanange huu huwa ni ishara ya ufunguzi wa ligi mbili za bara hili [Europa na Ligi ya mabingwa].
FC Barcelona inaingia katika mtanange wa leo ikiwa kama bingwa wa ligi ya mabingwa huku FC Sevilla ikiingia kama ligi wa Europa.
Tadhimini fupi kuelekea mchezo huo;Tangu mwaka 2010 vilabu hivi vimekutana mara 12 na katika mara zote hizo FC Sevilla haijawahi kuibuka mshindi mbele ya FC Barcelona,Je leo itakuwaje?
Mchezo huo utapigwa katika dimba hili liitwalo Georgia, Boris Paichadze Dinamo Arena.
VIKOSI
Barcelona XI: Ter Stegen; Alves, Pique, Mascherano, Mathieu; Busquets, Rakitic, Iniesta; Pedro, Suarez, Messi.
Sevilla XI: Rico; Mariano, Coke, Krychowiak, Trémoulinas; Banega, Krohn-Dehli; Reyes, Iborro, Konoplyanka; Gameiro.
Unai Emery kocha wa Sevilla
NYOTA WATAKAOKOSA MTANANGE HUO
Neymar,Jordi Alba na Douglas huku Sevilla wao wataikosa huduma ya kiungo Steven Nzonzi anayeumwa tumbo,huku mlinzi Adil Rami na Ciro Immobile wakiwa mguu ndani mguu nje kuwemo katika mtanange huo.
0 comments:
Post a Comment