728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, August 12, 2015

    USAJILI:SHAQIRI ASAINI STOKE CITY,AC MILAN YAFANYA KWELI ITALIA,VALBUENA AREJEA UFARANSA

    Pilika pilika za usajili zimeendelea kushika kasi barani Ulaya kwa wachezaji na makocha kuhama toka kilabu kimoja na kwenda kingine.

    Leo klabu ya Stoke City imeendelea kukiimarisha kikosi chake baada ya kuinasa saini ya winga hatari Xherdan Shaqiri,23 toka klabu ya Inter Milan kwa ada ya rekodi ya £12m.Shaqiri amesaini mkataba wa miaka mitano kuichezea Stoke City baada ya mambo kumuendelea kombo Italia.

    Klabu ya AC Milan imefanikiwa kumsajili mlinzi Alessio Romagnoli,20 toka AS Roma kwa kitita cha €28m 
    Baada ya kucheza soka Urusi kwa kipindi cha msimu mmoja tu winga Mathieu Valbuena,30 amerudi nyumbani kwao Ufaransa na kujiunga na klabu ya Olympique Lyonnais kwa kitita cha £3.5m akitokea Dynamo Moscow
    Baada ya kutemwa na klabu ya Juventus mwishoni mwa msimu uliopita hatimaye kiungo Simone Pepe,27 amejiunga na klabu ya Chievo Verona akiwa kama mchezaji huru.Pepe amesaini miaka minne
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: USAJILI:SHAQIRI ASAINI STOKE CITY,AC MILAN YAFANYA KWELI ITALIA,VALBUENA AREJEA UFARANSA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top