Klabu ya Azam FC imetwaa ubingwa wa kombe la Kagame baada ya kuifunga Gor Mahia kwa magoli 2-0 katika mchezo mkali wa fainali uliopigwa jioni ya leo katika uwanja wa taifa,Dar es Salaam.
Magoli ya Azam yamefungwa na John Bocco dakika ya 16 akiunganisha vyema krosi ya Kipre Tchetche huku dakika ya 64 Kipre Tchetche akiifungia Azam FC goli la pili kwa mkwaju wa faulo uliomuacha kipa wa Gor Mahia Boniphase Oluoch akichupa bila mafanikio.
Kufuatia ushindi huo Azam FC wanaweka kibindoni kiticha cha dola elfu 30,000 huku Gor Mahia wakipata dola 20,000.
0 comments:
Post a Comment