728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, June 11, 2017

    MABINGWA:Madogo wa England watwaa kombe la dunia la U-20


    Korea Kusini.

    TIMU ya taifa ya vijana ya England ya wachezaji we ye umri wa chini ya miaka 20 mchana wa leo imetwaa ubingwa wa kombe la dunia la vijana wa umri huo baada ya kuwafunga vijana wenzao wa Venezuela kwa bao 1-0 katika mchezo mkali wa fainali uliochezwa huko nchini Korea Kusini.

    Bao pekee la mchezo huo limefungwa katika dakika ya 35 na kinda wa klabu ya Everton,Dominic Calvert-Lewin na kuipa England ubingwa wake wa kwanza mkubwa tangu mwaka 1966 ilipotwaa kombe la dunia la wakubwa.

    Aidha katika mchezo huo ilishuhudiwa Venezuela wakishindwa kupata bao la kusawazisha baada ya mkwaju wa penati uliopigwa na Adalberto Penaranda kudakwa kiustadi na mlinda mlango wa England,Freddie Woodman anayeichezea klabu ya Newcastle United.

    Aidha pia katika mchezo huo ilishuhudiwa mshambuliaji wa England Dominic Solanke akitwaa mpira wa dhahabu baada ya kuibuka mchezaji bora wa michuano hiyo.

    Tuzo hiyo iliwahi pia kutwaliwa na nyota kama Diego Maradona,Lionel Messi, Luis Figo,Paul Pogba na Sergio Aguero.Tuzo ya mlinda mlango bora imekwenda kwa Freddie Woodman wa England.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MABINGWA:Madogo wa England watwaa kombe la dunia la U-20 Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top