728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, June 11, 2017

    USAJILI:Bayern Munich yamsaini winga wa zamani wa Arsenal


    Munich, Ujerumani.

    MABINGWA wa kihistoria wa ligi ya Bundesliga,Bayern Munich muda mfupi uliopita wametangaza kumsajili winga wa zamani wa Arsenal,Serge Gnabry.

    Taarifa iliyoweka kwenye mtandao wa Bayern Munich umesema Gnabry mwenye umri wa miaka 21 ameingia kandarasi ya miaka mitatu akitokea Werder Bremen kwa ada ya Euro Milioni 8.

    Gnabry alijiunga na Werder Bremen msimu uliopita baada ya kushindwa kujihakikishia nafasi ya kudumu kwenye kikosi cha Arsenal kinachonolewa na Mfaransa,Arsene Wenger.

    Akiwa na Werder Bremen msimu uliopita Gnabry aligeuka staa mkubwa baada ya kuifungia timu hiyo mabao 11 katika michezo 27 ya ligi ya Bundesliga.Mabao 10 kati ya 11 aliyafunga kwenye viwanja vya ugenini.Pia aliibuka mfungaji kwenye michuano ya Olimpiki ambapo alifunga mabao sita na kuiwezesha Ujerumani kushika nafasi ya pili nyuma ya Brazil waliokuwa mabingwa.

    Gnabry anakuwa mchezaji wa tatu kujiunga na Bayern Munich katika kipindi hiki cha majira ya joto.Wengine ni Sebastian Rudy na Niklas SĂĽle.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: USAJILI:Bayern Munich yamsaini winga wa zamani wa Arsenal Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top