Saudi Arabia.
JEZI ya Barcelona yenye nembo ya shirika la ndege la nchi ya Qatar,Qatar Airways siyo dili tena nchini Saudi Arabia hii ni baada ya serikali ya nchini hiyo ya Kiislamu kutangaza kuwa itatoa adhabu ya faini pamoja na kifungo cha miaka 15 kwa shabiki atakayeonekana amevaa jezi hiyo.
Hatua hiyo imekuja baada ya hivi karibuni nchi za kiarabu ikiwemo Saudi Arabia kuvunja uhusiano wa kidiplomasia na Qatar kufuatia nchi hiyo kuripotiwa kuwa na mahusiano ya karibu na kundi la kigaidi la ISIS.
Kwa mujibu wa mtandao wa Sky Italia,habari zinasema kuanzia sasa shabiki yoyote atakayeonekana hadharani amevaa jezi ya Barcelona yenye nembo ya Qatar Airways ama kumiliki bidhaa yoyote yenye uhusiano na nchi ya Qatar atakabiriwa na hatari ya kulimwa faini ya €135,000 pamoja na kifungo kitakachofikia miaka 15 jela.
Wakati huohuo habari zaidi zinasema katazo la kutumia bidhaa zenye uhusiano na nchi ya Qatar huenda likatangazwa pia katika nchi za falme za kiarabu,Misri na Yemen.
0 comments:
Post a Comment