728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, June 11, 2017

    TFF yatangaza tarehe ya kuanza zoezi la usajili wa wachezaji kwa vilabu vya ligi kuu,ligi daraja la kwanza


    Dar Es Salaam,Tanzania.

    Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), linatangaza kufungua dirisha la usajili kwa wachezaji wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Ligi Daraja la Kwanza na Ligi Daraja la Pili ikiwa ni ufunguzi wa msimu mpya wa mashindano wa 2017/2018.

    Dirisha hilo linafunguliwa Juni 15,mwaka huu na litafungwa Agosti 6,mwaka huu hivyo kila timu inayoshiriki michuano tajawa hapo juu, inaarifiwa kufuata kalenda hiyo ambayo tunaitangaza sasa.

    Tahadhali, hakutakuwa na muda wa nyongeza kwa timu ambazo hazitakamilisha usajili kama ilivyotokea msimu uliopita kwa baadhi ya timu kushindwa kufanya kusajili kwa wakati na dirisha likafungwa.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: TFF yatangaza tarehe ya kuanza zoezi la usajili wa wachezaji kwa vilabu vya ligi kuu,ligi daraja la kwanza Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top