728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, June 12, 2017

    USAJILI:Azam FC yaendelea na mavuno,yamnasa kipa wa Mbao FC


    Dar Es Salaam,Tanzania.

    KLABU Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC,imefanikiwa kumsajili wa aliyekuwa kipa wa Mbao, Benedict Haule.

    Haule amesaini mkataba wa miaka miwili utakaoanza kufanya kazi kuanzia Julai Mosi mwaka huu.

    Usajili huo unamfanya kipa huyo kurejea tena nyumbani ndani ya viunga vya Azam Complex, kwani aliwahi kulelewa katika kituo cha Azam Academy chini ya Kocha wa Makipa wa Azam FC, Idd Abubakar.

    Kipa huyo anaungana na makipa wengine wa Azam FC,Mwadini Ally na Metecha Mnata,tayari kabisa kuanza mchakamchaka wa kujiandaa na msimu ujao kuanzia Julai 3 mwaka huu.

    Huo ni usajili wa nne kwa Azam FC kuelekea msimu ujao 2017/2018,wengine ambao tayari saini zao zimenaswa ni kiungo nyota Salmin Hoza na washambuliaji wanaokuja kwa kasi Mbaraka Yusuph na Wazir Junior.



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: USAJILI:Azam FC yaendelea na mavuno,yamnasa kipa wa Mbao FC Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top