Kampala,Uganda.
TIMU ya taifa ya Uganda imefanikiwa kufuzu michuano ya AFCON baada ya jioni ya leo kuifunga timu ya taifa ya Comoro kwa bao 1-0 katika mchezo mkali wa Kundi D uliochezwa katika uwanja wa Nelson Mandela uliopo jijini Kampala.
Bao la ushindi lililoipeleka Uganda kwenye michuano ya AFCON baada ya kusubiri kwa miaka 38 limefungwa dakika ya 34 ya kipindi cha kwanza na kiungo Farouk Miya anayechezea klabu ya Anderletch ya Ubelgiji.
Miya alifunga bao hilo baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Moses Oloya na kufumua mkwaju uliomshinda kipa wa Comoro,Ali Hamada.
Ushindi huo umeifanya Uganda kufuzu ikiwa kinara wa pamoja wa kundi D baada ya kufikisha pointi 13.Mara ya mwisho kwa Uganda kufuzu AFCON ilikuwa ni mwaka 1978.Timu nyingine ambayo imefuzu kutoka kundi hilo ni Burkina Faso ambayo imeichapa Botswana kwa mabao 2-1 na kufikisha pointi 13 sawa na Uganda.
Vikosi
Uganda Cranes XI : Denis Onyango (G.K),Nicholas Wadada, Joseph Ochaya, Isaac Isinde, Murushid Jjuuko, Khalid Aucho,Tonny Mawejje, Moses Oloya, Geoffrey Massa (Captain), Farouk Miya na William Luwagga Kizito
Comoros XI:Ali Hamada (G.K), Abdou Nadsm, Fouad Bachirou, Mohamed El Fardou, Yousseouf Mchangama, Bakar Djamel, Ahamada Kassim, Ahamadi Kombo, Ben Youssouf,
Chamed Nasser, Youssouf Madi
0 comments:
Post a Comment