Uyo,Nigeria.
NAHODHA wa Taifa Stars,Mbwana Ally Samata amesifu kiwango kilichoonyeshwa na timu hiyo licha ya kufungwa bao 1-0 na Nigeria katika mchezo wa mwisho wa kundi G wa michuano ya kuwania tiketi ya AFCON.
Samatta ambaye jana Jumamosi alikuwa mwiba mchungu kwa mabeki wa Nigeria alikiambia kituo cha Complete Sports cha Nigeria kuwa anajivunia kandanda safi lililoonyeshwa na Taifa Stars na kusisitiza kuwa siku za usoni matokeo hayatakuwa kama yale yaliyopatikana Akwa Ibom kwa Stars kulala kwa kwa bao moja lililofungwa na Kelechi Iheanacho dakika ya 77.
Wakati huohuo Samatta amewaponda mabeki wa Nigeria na kudai kuwa walikuwa wakicheza kitemi sana na mwamuzi Mehdi Abid Charet alishindwa kuwapa Stars ulinzi wa kutosha.
“Mabeki wenu walitukamia na walikuwa wakicheza kitemi sana,mwamuzi alipaswa kutupa ulinzi zaidi.Matokeo yoyote ya mchezo wetu yalikuwa hayana msaada kwa timu zote mbili sasa kwanini tuuane?Alihoji Samatta kwa hasira.
Pia Samatta alitumia fursa hiyo kumzungumzia Wilfred Ndindi mchezaji mwenzie katika klabu ya KRC Genk ambaye jana alikuwa akiichezea Nigeria mchezo wa kwanza wa kimataifa.
“Ndidi ni mtu mzuri.Niliongea nae mambo mengi kabla ya mchezo huu.Nashukuru tumemaliza salama,tunarejea Ubelgiji kuitumikia klabu yetu ya KRC Genk.
0 comments:
Post a Comment