728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, September 04, 2016

    OZIL AMTAKA UBAYA JACK WILSHERE ARSENAL


    Munich,Ujerumani.

    MESUT Ozil amemtaka ubaya nyota mwenzie wa Arsenal,Jack Wilshere, baada ya kuanza kuitaka jezi Namba 10 iliyokuwa ikivaliwa na nyota huyo aliyehamia Bournemouth kwa mkopo wa msimu mmoja.

    Ozil,27,ambaye hivi karibuni amepewa jezi namba 10 katika timu yake ya taifa ya Ujerumani baada ya Lukas Podolski kustaafu amekiambia kituo cha Televisheni cha Sport1 kwamba anataka pia kuivaa namba hiyo katika klabu yake ya Arsenal.




    'Kweli naitaka jezi hiyo na nimeishawaambia wahusika.Kwangu jezi namba 10 ina maana kubwa sana.Ndiyo namba ninayoipenda kuliko namba zote na zaidi ya yote ndiyo namba ninayoicheza.Ni namba iliyovaliwa na magwiji kama Zinédine Zidane,Diego Maradona na Pelé.

    Kabla ya Wilshere jezi namba 10 katika klabu ya Arsenal ilikuwa ikivaliwa na wakali kama Dennis Bergkamp na Robin Van Persie.

    Kwa sasa Ozil anavaa jezi namba 11 Arsenal hivyo ni jambo la kusubiri na kuona kama atapewa jezi hiyo.

    Je,Wilshere atasema nini baada ya kumaliza uhamisho wake wa mkopo Bournemouth?


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: OZIL AMTAKA UBAYA JACK WILSHERE ARSENAL Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top