728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, September 04, 2016

    TAIFA STARS YAJAZWA NOTI NA SERIKALI YA NIGERIA

    Uyo,Nigeria.

    SERIKALI ya jimbo la Akwa Ibom imeipa timu ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' Kitita cha pesa za Nigeria ,Naira Millioni 5 ambazo ni sawa na Dola 10,000 za Marekani kama asante ya kukubali kucheza katika jimbo hilo lenye utajiri mkubwa wa nishati ya mafuta.

    Pesa hiyo imetolewa na Gavana wa jimbo la hilo,Emmanuel Odom, ambaye pia alikuwa mgeni rasmi katika mchezo huo ulioisha kwa Taifa Stars kulala kwa bao 1-0 kutoka kwa wenyeji Nigeria katika mchezo wa mwisho wa kundi G wa kuwania tiketi ya kufuzu michuano ya AFCON 2017 nchini Gabon.

     Wakati Taifa Stars ikipata kiasi hicho cha pesa,Nigeria,ambao walikuwa washindi katika mchezo huo wameweka kibindoni kitita cha Naira Millioni 10 ambazo ni sawa na Dola 25,000 za Marekani.

    Hatua hiyo ya Jimbo la Akwa Ibom imekuja kama ahueni wachezaji kwa Nigeria ambao kabla ya mchezo huo walitaarifiwa na chama cha soka cha nchi hiyo NFF kuwa hawatapewa bonusi yoyote kutokana na chama hicho kutokuwa na pesa wakati huu na badala yake kitawagharamia tiketi za ndege za kurudi katika vilabu vyao.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: TAIFA STARS YAJAZWA NOTI NA SERIKALI YA NIGERIA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top