728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, August 13, 2016

    YANGA SC YAPATA USHINDI WA KWANZA SHIRIKISHO YAIGONGA MO BEJAIA 1-0 U/TAIFA


    Dar Es Salaam,Tanzania.

    BAADA ya kushindwa kupata ushindi katika michezo minne mfululizo hatimaye leo Yanga SC imepata ushindi wake wa kwanza baada ya jioni ya hii kuichapa Mo Bejaia kwa jumla ya bao 1-0 katika mchezo mkali wa kundi A wa kombe la Shirikisho uliochezwa katika uwanja wa taifa,Dar Es Salaam.

    Bao pekee la mchezo huo limefungwa dakika ya 3 ya kipindi cha kwanza na Mshambuliaji,Amissi Tambwe,baada ya kumalizia mpira wa kichwa uliopigwa na Winga,Simon Msuva.

    Yanga SC watapaswa kujilaumu Kwani licha ya kufika mara nyingi langoni mwa Mo Bejaia lakini walishindwa kufunga.

    Aidha katika mchezo huo Yanga SC iliwapoteza walinzi wake wa wili Andrew Vincent "Dante" na Juma Abdul kutokana na majeruhi na nafasi zao kuchukuliwa na Kevin Yondani pamoja na Juma Said Makapu.

    Matokeo hayo yameifanya Yanga SC kufikisha alama nne katika michezo mitano huku Mo Bejaia ikibaki na alama zake tano katika michezo mitano.

    VIKOSI

    Yanga SC;

    Ally Mustafa ‘Dida’, Juma Abdul, Mwinyi Mngwali, Andrew Vincent ‘Dante’, Vincent Bossou, Mbuyu Twite, Simon Msuva, Thabani Kamusoko, Amissi Tambwe, Obrey Chirwa na Deus Kaseke.

    MO Bejaia;

    Chamseddine Rahmani, Ismail Benettayeb,Faouzi Rahal, Sofiane Khadir, Soumaila Sidibe, Zakaria Bencherifa, Mohamed Yacine Athmani, Morgan Betorangal, Sofiane Baouali,Amar Benmelouka na Kamel Yesli.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: YANGA SC YAPATA USHINDI WA KWANZA SHIRIKISHO YAIGONGA MO BEJAIA 1-0 U/TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top