Dar Es Salaam,Tanzania.
SASA ni rasmi kuwa Mshambuliaji wa Kimataifa wa Burundi,Laudit Mavugo,ataichezea Simba SC katika michuano ya Ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara pamoja na ile ya Kombe la Shirikisho (FA) hii ni baada ya leo mchana klabu hiyo yenye makao yake makuu Msimbazi,Dar Es Salaam kupokea hati yake ya uhamisho wa kimataifa ( ITC ).
Mbali ya Mavugo mshambuliaji mwingine wa klabu hiyo aliyekuwa na hatihati ya kuikosa michezo ya mwanzo ya Ligi kuu ni Muivory Coast,Frederic Blagnon,lakini nae ITC yake imepatikana.
Kuwasili kwa hati hizo kunawapa Simba SC uhalali wa kuwatumia wachezaji hao katika michuano yote itakayoihusisha klabu hiyo ambayo msimu huu imepania kutwaa ubingwa wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara
Mavugo alisajiliwa na Simba SC hivi karibuni baada ya kumaliza mkataba katika klabu ya Vital’o huku Blagnon akijiunga kutoka kwa miamba ya Ivory Coast,Africa Sports.
0 comments:
Post a Comment