728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, August 20, 2016

    IBRAHIMOVIC APIGA MBILI NA KUIPELEKA MAN UNITED KILELENI ENGLAND.


    Manchester, Uingereza.

    Zlatan Ibrahimovic amefunga mabao mawili na kuiwezesha Manchester United kukalia kwa muda kiti ya uongozi wa ligi kuu ya Uingereza baada ya usiku huu kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Southampton.

    Katika mchezo huo uliochezwa katika uwanja wa Old Trafford na kushuhudiwa na watazamaji 75,326,Ibrahimovic alianza kuifungia Manchester United bao la kwanza kwa kichwa dakika ya 36 ya kipindi cha kwanza akiunganisha krosi ya nahodha Wayne Rooney toka winga ya kulia.

    Ibrahimovic aliiandikia Manchester United bao la pili dakika ya 52 kwa mkwaju wa penati uliopatikana baada ya kiungo wa Southamp,Jodie Clasie kumwangusha Luke Shaw ndani ya boksi.

    Aidha katika huo mchezaji ghali zaidi duniani kwa sasa Paul Pogba kwa mara ya kwanza alipata nafasi ya kuichezea klabu baada ya kuanza katika kikosi cha kwanza.

    Matokeo hayo yanaifanya Manchester United iwe kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ikiwa imejikusanyia pointi sita katika michezo miwili.



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: IBRAHIMOVIC APIGA MBILI NA KUIPELEKA MAN UNITED KILELENI ENGLAND. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top