728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, August 02, 2016

    EVERTON YAMNASA GUEYE

    Liverpool,England.

    KLABU ya Everton imekamilisha usajili wa kiungo wa Senegal,Idrissa
    Gueye,kwa kandarasi ya miaka minne kutoka klabu ya Aston Villa kwa ada ya uhamisho £7.1m.

    Everton imemsajili Gueye,26,baada ya kuvutiwa nae tangu alipojiunga na Aston Villa mwezi Agosti mwaka jana 
    akitokea Lille ya Ufaransa kwa dau la £5m.

    Gueye ameiacha Aston Villa baada ya kuichezea michezo 38 ya ligi kuu England katika kipindi cha msimu mmoja alichohudumu katika klabu hiyo ya Midlands.

    Mwaka 2011,Gueye,aliisaidia Lille kutwaa ubingwa wa ligi daraja la kwanza nchini Ufaransa (Ligue 1).Lille iliyokuwa na nyota kama Mathieu Debuchy,Eden Hazard na Gervinho.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: EVERTON YAMNASA GUEYE Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top