728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, August 16, 2016

    CHELSEA YAANZA MSIMU MPYA KWA USHINDI


    London,England.

    CHELSEA imeanza msimu mpya wa ligi kuu England kwa tabasamu baada ya Jumatatu Usiku kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 katika mchezo safi uliochezwa katika uwanjs wa Stamford Blidge.

    Katika mchezo huo uliochezeshwa na mwamuzi ,Antony Taylor,Chelsea ndiyo iliyokuwa ya kwanza kupata bao baada ya Eden Hazard kufunga kwa mkwaju wa penati dakika ya 47 kufuatia Cesar Azpilicueta kuangushwa ndani ya boksi na Michail Antonio.

    West Ham walisawazisha dakika ya 77 kupitia kwa beki wake,James Collins, lakini Chelsea wakajihakikishia ushindi baada ya Diego Costa kufunga bao dakika ya 89 kwa mkwaju mkali wa mita 20.

    VIKOSI:

    Chelsea:

    Courtois; Ivanovic, Cahill, Terry,Azpilicueta; Kante; Willian, Matic, Oscar,Hazard; Costa

    Akiba: Begovic, Aina, Fabregas, Loftus-Cheek, Moses, Pedro,Batshuayi

    West Ham:

    Adrian, Antonio, Reid, Collins, Masuaku,Nordtveit, Ayew, Noble, Kouyate, Valencia,Carroll

    Akiba: Randolph, Byram, Ogbonna,Obiang, Oxford, Tore, Payet


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: CHELSEA YAANZA MSIMU MPYA KWA USHINDI Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top