728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, July 07, 2016

    HUYU NDIYE CRISTIANO RONALDO USIKU MMOJA REKODI 4 KUBWA ULAYA

    Lyon,Ufaransa.

    ANAITWA Cristiano Ronaldo!!Acha na habari ya Ureno kutinga Fainali ya Euro 2016 kwa kuibwaga Wales kwa mabao 2-0 huko Lyon,Ufaransa.

    Habari nyingine kubwa ni Nahodha wake Cristiano Ronaldo,31, kuweka rekodi kubwa Ulaya ambazo ni hizi zifuatazo!!

     *Bao moja alilofunga Jumatano Usiku dhidi ya Wales limemfanya afikishe mabao tisa na kumfanya aifikie rekodi ya gwiji wa zamani wa Ufaransa,Michel Platini ya kuwa mfungaji bora wa muda wote wa Euro.Tofauti ni kwamba,Platini,alifunga bao zote tisa katika fainali za Euro za mwaka 1984.

    *Pia Ronaldo amekuwa mchezaji wa kwanza kufunga bao katika fainali nne tofauti za Euro

    *Ronaldo amecheza jumla ya michezo 20 katika michuano hiyo ikiwa ni idadi kubwa zaidi kupita wachezaji wote katika historia ya michuano hiyo mikubwa zaidi Ulaya.

    *Ronaldo pia ni mchezaji wa kwanza kuwahi kucheza nusu fainali tatu za michuano ya Euro kabla yake hakuna aliyewahi kuweka rekodi hiyo.

    Huyu ndiye Cristiano Ronaldo.....!!



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: HUYU NDIYE CRISTIANO RONALDO USIKU MMOJA REKODI 4 KUBWA ULAYA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top