LONDON,ENGLAND.
Arsenal imefufua matumaini ya kuendelea kuwemo kwenye mbio za kuwania ubingwa wa ligi kuu England baada ya jioni ya leo kuitandika Bournemouth kwa mabao 2-0 huko Vitality.Mabao yaliyoipa Arsenal ushindi yamepatikana dakika za 23 na 24 kupitia kwa Mesut Ozil na Alex Oxlade Chamberlain ambaye kabla ya leo alikuwa hajafunga bao katika mchezo wa ligi kuu kwa kipindi cha miezi 16.
Kufuatia ushindi huo Arsenal imepanda mpaka nafasi ya 3 baaada ya kufikisha pointi 48 ikiwa nyuma ya Tottenham iliyo katika nafasi ya pili kwa tofauti ya magoli ya kufunga.
0 comments:
Post a Comment