728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, October 05, 2015

    SIFA TU:BAADA YA LIVERPOOL KUMTIMUA RODGERS,BARCA YAJIPANGA KUIFANYIA KITU MBAYA

    Barcelona,Hispania.

    Barcelona inataka kuipiga bao Liverpool kwa kumsajili kiungo wake Mbrazil Phillipe Coutinho hasa baada ya klabu hiyo ya England kumtupia virago aliyekuwa kocha wake Brendan Rodgers hapo jana jumapili.

    Barcelona inataka kutumia mwanya wa kutimuliwa kwa Rodgers ili kumnasa Coutinho,23 hapo mwezi januari 2016 ambaye alikuwa ni kipenzi kikubwa cha kocha huyo aliyedumu Liverpool kwa misimu mitatu tu.

    Habari kutoka katika gazeti la michezo la Hispania la Sport zinasema Barcelona inajiandaa kutuma ofa ya £23m hapo mwezi januari pindi adhabu yake ya kutofanya usajili itakapokuwa imefikia mwisho.Barcelona inataka kukiimarisha kikosi chake kwa kusajili mchezaji ambaye anaweza kuchezesha timu,kutengeneza nafasi za mabao na kufunga sifa ambazo Coutunho anazo.

    Coutinho alisajiliwa na Brendan Rodgers msimu wa 2012-2013 akitokea Inter Milan kwa ada ya £8.5m hivyo kuondoka kwa kocha huyo kunatarajiwa kutairahisishia kazi klabu ya Barcelona katika mbio zake za kumnasa kiungo huyo wa kimataifa wa Brazil.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: SIFA TU:BAADA YA LIVERPOOL KUMTIMUA RODGERS,BARCA YAJIPANGA KUIFANYIA KITU MBAYA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top