728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, October 05, 2015

    HAKUNA KAMA IBRAHIMOVIC PSG,AVUNJA REKODI YA MABAO,AKOMBA TUZO.

    Paris,Ufaransa.

    Mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic jana jumapili alitawazwa kuwa mfungaji bora wa muda wote wa klabu ya PSG baada ya kuifungia klabu hiyo magoli mawili katika mchezo wa ligi ya Ufaransa (Ligue 1) ambapo PSG iliibuka na ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Marseille.

    Kufuatia magoli hayo mawili yaliyoendelea kuibakisha PSG kileleni mwa ligi hiyo,Ibrahimovic amekabidhiwa tuzo baada ya kufikisha magoli 110 katika michezo 127 na kuivunja rekodi ya magoli 109 iliyokuwa ikishikiliwa na Mreno Pauleta.

    Baada ya kutwaa tuzo hiyo Ibrahimovic ambaye mkataba wake unaisha juni 2016 alisema kiu yake ni kuendelea kuandika historia akiwa na miamba hiyo ya Ufaransa.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: HAKUNA KAMA IBRAHIMOVIC PSG,AVUNJA REKODI YA MABAO,AKOMBA TUZO. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top